Supported Content
Bwana Nimerudi tena by PRAISE TEAM TAG FOREST YA KWANZA
Bwana, Nimerudi tena, Yesu nakushukuru,
Wenginge sijui, ila mimi Bwana,
Nimejua umenitendea
Bwana, Nimerudi tena, Yesu nakushukuru,
M enginge sijui, ila hili Bwana,
Nimejua umenitendea,
Nimeomba mengi, umenijibu moja,
Umetutendea wengi, mimi nimerudi,
Japo mengine bado,
Ila natambua, Thamani ya hili moja,
Wale wengine kenda, mimi sijui,
Ila nachojua, kwangu umetenda,
Mengine sijui, nimejua umenitendea,
Mimi ni Msamaria tu, mtu wa makabila mengine,
Wala sikustahili haya uliyonitendea
Wengine sijui wanaona nini,
Ila mimi bwana ninauona wema wa ajabu,
Wenye ukoma tulikuwapo,
na neno lako halikufanya makosa,
Wengine sijui ila mimi bwana,
Nimejua umenitendea
Wenye dhambi, tulikuwa wengi
Na damu yako ikanitakasa
Wengine sijui ila mimi bwana
Nimejua umenitendea
Utukufu kwako tu,
na heshima zote, kwako tu
Umenitenda wema,
Umenitenda vyema
Umenitendea wema mkuu
Umenitenda wema,
Umenitenda vyema
Umenitendea wema mkuu
Support Praise Team TAG by liking, sharing, and subscribing to their YouTube channel. Also, listen to their song, Bwana Nimerudi Tena below: